Jumatano 9 Julai 2025 - 21:31
Umuhimu wa kutambua nyakati kwa mtazamo wa Sheikh Ibrahim Zakzaky

Hawzah/ Ayatollah Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema: “Hata kama chaguo la mwisho katika njia ya muqawama ni kufa kishahidi, bado hiyo ni furaha kubwa zaidi, kama alivyochagua Imam Hussein (as) katika njia ya kuutetea Uislamu.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, sambamba na siku za maombolezo ya Sayyid al-Shuhada (as), katika hotuba aliyotoa mbele ya wapenda Ahlulbayt (as) na wapenzi wa Nyumba ya Ismah na Toharah huko Nigeria, alizungumzia juu ya utukufu wa Imam Hussein (as) na thamani ya kusimama dhidi ya madhalimu na mabaradhuli wa kidunia.

Sheikh Zakzaky alisifu thamani ya mambo kama vile kusimama kidete na kuwa madhubuti mbele ya dhulma na uonevu, na akaongeza kuwa: “Hata kama chaguo la mwisho katika njia ya muqawama ni kufa kishahidi, bado hiyo ni furaha kubwa zaidi, kama alivyochagua Imam Hussein (as).”

Aliendelea kusema kuwa:

“Katika historia, mara zote kundi la haki limekuwa likipigana dhidi ya kundi la batili, kama vile Firauni na Nabii Musa, na mapambano mengine mengi baina ya haki na batili ambayo daima yamekuwa yakikabiliana. Imam Hussein (as) alipambana na Yazid wa wakati wake, na leo sisi pia tunapaswa kumtambua Yazid wa wakati wetu, na tuwe upande sahihi wa historia kwa kuzingatia mafundisho ya Imam Hussein (as).”

Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha